#Local News

MATHARE UNITED YATULIZA HOFU BAADA YA VIPIGO RWANDA

Kocha wa Mathare United David Ouma amekataa kuingiwa na hofu baada ya timu yake kupoteza mechi zote tatu na kushindwa kufunga bao katika ziara ya maandalizi nchini Rwanda.

Mathare ilipoteza kwa mabao 1-0 dhidi ya APR FC, 1-0 dhidi ya Gorilla FC na 3-0 dhidi ya Rayon Sports katika kipindi cha siku nane, huku Ouma akisema matokeo hayo yamewapa kipimo muhimu kabla ya msimu mpya.

Ouma amesema kiwango cha wapinzani nchini Rwanda kimeisaidia timu kubaini maeneo yenye udhaifu na kuyafanyia kazi, huku akilenga kujenga upya kikosi kilichomaliza nafasi ya 14 msimu uliopita.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *