IPOA YACHUNGUZA KIFO CHA MFUNGWA NAIROBI
Maafisa wa polisi na mamlaka ya IPOA wameanzisha uchunguzi baada ya mwanaume mmoja aliyekuwa amekamatwa na kuzuiliwa katika celi za kamukunji jijini Nairobi kuaga dunia.
Mwanaume huyo kwa jina Mutembei alianguka na kuzirai akiwa katika celi kabla ya kukimbizwa katika hosipitali ya kitaifa ya Kenyatta kabla ya kuaga dunia.
Mtembei alikuwa amekamatwa na kuzuiliwa kwa madai ya kutoa fujo eneo la kamukunji.
Mwili wake umepelekwa katika hifadhi ya maiti ukisubiri kufanyiwa upasuaji.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































