MUTURI:WAFANYIKAZI WA UMMA HAWANA UELEWA WA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA
Asilimia kubwa ya wafanyikazi wa umma wanaendelea kukumbana na changamoto za ukosefu wa uelewa wa maytumizi ya teknolojia ya mawasiliano ICT.
Waziri wa huduma za umma Justine Muturi akizungumza katika kaunti ya Mombasa amesema kuwa ipo haja ya wafanyikazi wote wa uma kupewa mafunzo kuhusiana na matumizi ya teknolojia ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma.
Muturi aidha amezitaka idara mbali mbali za serikali kuhakikisha huduma zao zinapatikana katika vituo vya huduma center.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































