IEBC YATAKA SHILINGI BILIONI 74 KWA UCHAGUZI WA 2027
Uchaguzi wa mwaka 2027 huenda ukawa wa gharama kubwa zaidi, huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, ikiwasilisha ombi la takriban shilingi bilioni 74 kwa Hazina ya Kitaifa ili kugharamia maandalizi ya uchaguzi mkuu
Kamishna wa IEBC, Ann Nderitu, amesema ongezeko la idadi ya wapiga kura waliojiandikisha limekuwa kichocheo kikuu cha ongezeko la gharama, huku bajeti hiyo ikijumuisha ununuzi wa teknolojia mpya ya uchaguzi na karatasi za kura
Nderitu amesema teknolojia mpya ya uchaguzi inatarajiwa kugharimu takriban shilingi bilioni 10, huku ununuzi wa karatasi za kura ukikadiriwa kufikia shilingi bilioni 6.8, katika bajeti iliyowasilishwa kwa Hazina.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































