#Local News

WANAFUNZI WAREJEA SHULENI, SAKATA LA UFADHILI LAENDELEA

Wanafunzi wameanza muhula wa tatu leo huku shule zikiingia katika muhula mpya na swali la ufadhili wa serikali likiendelea kutatiza, licha ya Rais William Ruto kusema shilingi bilioni 18 tayari zimetolewa kugharamia mahitaji ya shule.

Hata hivyo, wadau wa elimu wanapinga madai hayo wakisema wakuu wa shule bado hawajapokea fedha hizo, hali inayowaacha shule katika changamoto za kugharamia shughuli muhimu za masomo.

Muungano wa KUPPET, umesema wakuu wa shule wanaweza kulazimika kuwaomba wazazi kuchangia fedha zaidi ili kuziba pengo la ufadhili, huku shule zikikabiliwa na presha ya kuendesha shughuli zao.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

WANAFUNZI WAREJEA SHULENI, SAKATA LA UFADHILI LAENDELEA

RUTO: SIHOFII WAPINZANI WANGU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *