NDINDI NYORO AMTAKA MURKOMEN KUJIUZULU
Kiongozi wa chama cha PPK, Ndindi Nyoro, amemtaka Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, kujiuzulu akisema serikali imeshindwa kudhibiti kuongezeka kwa vurugu katika mikutano ya kisiasa nchini
Akizungumza katika kaunti ya Murang’a Nyoro amesema licha ya serikali kuahidi kuwachukulia hatua wahusika na wafadhili wa ghasia hizo, hakuna aliyekamatwa hadi sasa
Amesisitiza kuwa upinzani utaendelea kuwa na umoja kwa lengo la kushinda uchaguzi mkuu wa 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































