#Local News

RUTO: SIHOFII WAPINZANI WANGU

Rais William Ruto amewapuuza wapinzani wake kisiasa akisema hana hofu nao kuelekea uchaguzi mkuu, akiamini Wakenya wataweza kutofautisha kati ya porojo za kisiasa na mipango ya kuendeleza nchi.

Ruto amesema wapinzani wake wanapaswa kuwaeleza Wakenya watakachofanya kwa vitendo badala ya kutumia matusi, kauli za kejeli na misemo ya kisiasa katika kampeni zao.

Rais amesema ana imani na busara za wapiga kura wa Kenya katika kufanya uamuzi, akiwataka wapinzani wake kuwasilisha sera na njia mbadala za kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *