#Local News

UHURU: SITAKI KUITWA “SPONSOR”

Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta amewataka wanasiasa kuacha kutumia nguvu kuzuia mikutano ya wapinzani kuelekea uchaguzi wa 2027, akisema badala yake wajielekeze kuuza sera na ilani zao kwa Wakenya

Akizungumza katika Kaunti ya Trans Nzoia Uhuru amesema wananchi wanapaswa kupewa uhuru wa kuamua viongozi wanaowataka, bila wanasiasa kuwazuia wapinzani wao kufanya mikutano

Uhuru pia amekanusha madai kuwa kurejea kwake hadharani kunaashiria kurudi katika siasa za ushindani, akisema hana mpango wa kuwania nafasi yoyote na hataki kuitwa “mfadhili” wa kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

UHURU: SITAKI KUITWA “SPONSOR”

RUTO: SIHOFII WAPINZANI WANGU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *