#Rugby #Sports

KABRAS YATWAA TAJI LA DRIFTWOOD 7S

Kabras Sugar imefanya mabadiliko ya kuvutia na kutwaa taji la Driftwood 7s baada ya kuwashinda mabingwa watetezi KCB kwa alama 15-5 katika fainali kali iliyochezwa Mombasa Sports Club\.

KCB ilionekana kuelekea kutetea ubingwa baada ya Festus Shiasi kufunga jaribio dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza na kuwapa mabingwa hao uongozi wa 5-0 kabla ya mapumziko.

Lakini kipindi cha pili kiligeuza kila kitu, Kabras ikirejea kwa kasi na kufunga majaribio matatu ya haraka na kubadili matokeo hadi 15-5 na hivyo kujinyakulia ubingwa wa Driftwood 7s kwa kishindo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *