#Football #Sports

FKF SUPER CUP: TUSKER YAANZA MSIMU KWA KUINYAMAZISHA GOR MAHIA

Tusker FC imeanza msimu wa 2026/27 kwa kishindo baada ya kuilaza Gor Mahia 3-1 na kutwaa taji la FKF Super Cup katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Francis Oduor, Engine Ikutwa na Ian Simiyu ndio walioipa Tusker mabao yake huku Ikutwa pia akiifungia Gor Mahia bao la kufutia machozi dakika ya 38, matokeo yaliyoipa Tusker taji lake la kwanza msimu huu.

Super Cup imezikutanisha Gor Mahia, mabingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita, na Tusker, washindi wa FKF Cup, katika maandalizi ya mwisho kabla ya msimu mpya wa ligi kuanza wikendi ya Agosti 29.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *