BEI YA MBEGU ZA MAHINDI KUSHUKA KWA ASILIMIA 50 MWEZI UJAO.
Rais William Ruto ametangaza kuwa serikali itapunguza bei ya mbegu za mahindi kwa asilimia 50 kuanzia mwezi Septemba mwaka huu. Ruto amesema hatua hiyo itapunguza bei ya gunia la mbegu za mahindi kutoka bei ya sasa sokoni ya Shilingi 300 hadi Shilingi 150.
Akizungumza katika hafla ya ibaada, Kaunti ya Taita Taveta, Kiongozi wa Nchi pia amesema serikali itahakikisha wakulima wanatumia msimu ujao wa mvua fupi kupanda mahindi zaidi kufuatia mavuno duni msimu uliopita kutokana na ukosefu wa mvua.
Ruto aidha amesema serikali yake imeamua kutoa ruzuku ya Shilingi 500 kwa kila gunia la mbolea. Gunia ambalo lilikuwa likiuzwa kwa Shilingi 2,500 sasa litauzwa kwa Shilingi 2,000. Rais pia ametangaza kuwa Shilingi bilioni 18 za ruzuku ya wanafunzi tayari zimetolewa kwa shule, huku zikijiandaa kufunguliwa tena Jumatatu ijayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































