#Local News

MBUNGE WA MUKURWE-INI AFIKA MBELE YA NCIC

Mbunge wa Mukurwe-ini John Kaguchia amefika mbele ya Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano, NCIC, kujibu tuhuma za kutoa matamshi ya uchochezi.

Mawakili wa Kaguchia wameiambia tume hiyo kuwa matamshi ya mteja wao yalinukuliwa nje ya muktadha aliokusudia, wakisisitiza kuwa hakuwa na nia ya kueneza chuki au kuchochea mgawanyiko miongoni mwa Wakenya.

Kaguchia ameendelea na mchakato wa kujibu tuhuma hizo mbele ya NCIC, huku tume ikiendelea kuchunguza matamshi yanayodaiwa kuwa ya uchochezi.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *