FAMILIA ZA AJALI YA NDEGE DIANI KUSUBIRI
Familia za waathiriwa wa ndege iliyowaua watalii 10 ambao ni raia wa kigeni na rubani raia wa Kenya katika eneo la Diani mapema Jumanne zitasubiri kwa hadi siku 30 kabla ya kufahamu chanzo cha ajali hiyo.
Kulingana na katibu katika idara ya safari za angani Teresia Mbaika, muda huo utahitajika ili kukamilisha uchunguzi katika ajali hiyo, akiongeza kwamba wanaendelea kuondoa miili iliyokwama kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Ametoa hakikisho kuwa anga za Kenya ziko salama kwa wasafiri wote.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































