NCA YADAI JENGO HALIKUWA LIMESAJILIWA
Imebainika kwamba jengo lililoporomoka mtaani Karen jijini Nairobi Jumamosi iliyopita halikuwa limesajiliwa inavyohitajika kisheria.
Haya ni kulingana na mamlaka ya kitaifa inayosimamia mijengo NCA, ikisema kuwa uchunguzi wa awali umeashiria dosari katika muundo wa jengo hilo la ghorofa moja lililoporomoka kutokana na uzito wa zege.
Watu wawili walifariki, wawili wakapata majeraha mabaya huku wengine 7 wakitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































