8-4-4 GRADE 10? WALIMU WATISHIA
Baadhi ya walimu wakuu katika shule za upili nchini wametishia kuanza kuwafunza wanafunzi wa gredi ya 10 kutumia vitabu vya mtaala wa zamani 8-4-4 kutokana na ukosefu wa vitabu vya gredi hiyo iliyo chini ya mtaala wa umilisi CBE.
Hii ni kutokana na hatua ya serikali kukosa kusambaza vitabu vya gredi hiyo hadi sasa, na hivyo masomo hayo kukosa kuanza katika nyingi ya shule za sekondari ya juu nchini.
Awali, serikali iliahidi kuwasilisha vitabu hivyo kufikia katikati mwa mwezi huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 













































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































