GUARDIOLA ATOA MAONI KUHUSU MUSTAKABALI WA GREALISH
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana uhakika kuhusu mustakabali wa mchezaji Jack Grealish, akisisitiza kuwa anamtakia kila la heri katika hatua yake ya sasa.
Guardiola amesema Grealish alikuwa na mchango mzuri alipokuwa akipata muda wa kucheza, akitaja pia athari yake katika msimu wa ushindi wa mataji matatu kwa klabu hiyo.
Ameongeza kuwa jeraha limemkosesha mwendelezo wa mchezo, lakini ana matumaini kuwa atapona na kurejea uwanjani msimu ujao kuendelea kucheza kwa kiwango chake cha juu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































