#Local News

VYAMA VYA KISIASA KUSAINI HATI YA AMANI

Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano Askofu Kepha Nyamweya amesema kila chama cha kisiasa kinatarajiwa kusaini hati ya amani kuelekea uchaguzi mkuu, hatua inayolenga kukuza utulivu na kuzuia migawanyiko ya kisiasa nchini

Nyamweya amesema pia kuna majadiliano ya kuhakikisha kila anayelenga kuwania nafasi ya kisiasa anapitia mchakato wa kuthibitishwa na NCIC, pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa

Amesema Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, huenda ikawa chombo cha mwisho kuidhinisha wagombea kabla ya kuruhusiwa kushiriki katika uchaguzi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *