#Local News

NCIC YAANZA KUWASAKA WACHOCHEZI WA GHASIA HOMA BAY

Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano NCIC imeanza kuchunguza watu wanaoshukiwa kuhusika na matamshi ya chuki na uchochezi yaliyosababisha kuvurugwa kwa mkutano wa Linda Mwananchi katika kaunti Homa Bay.

Mwenyekiti wa NCIC Askofu Kepha Nyamweya amesema tume hiyo inachukua hatua kubaini waliohusika na kauli na vitendo vilivyochangia kuvurugwa kwa mkutano huo huku akionya dhidi ya ghasia za kisiasa na migawanyiko ya kikabila kuelekea uchaguzi wa 2027.

Nyamweya amehoji sababu ya kutokea kwa tukio hilo akisisitiza kuwa kila Mkenya ana haki ya kikatiba kusafiri sehemu yoyote nchini na kuwasilisha maoni yake ya kisiasa kwa njia ya amani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

NCIC YAANZA KUWASAKA WACHOCHEZI WA GHASIA HOMA BAY

NDINDI NYORO AJIUNGA NA UPINZANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *