SERIKALI YATOA MUDA WA MIEZI TISA KUKAMILISHA VIWANJA NCHINI
Katibu Mkuu wa Michezo Elijah Mwangi amesema serikali inalenga kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu yote ya michezo inayoendelea nchini ndani ya miezi tisa ijayo
Mwangi amesema serikali ya kitaifa inashirikiana na serikali za kaunti kuhakikisha wanakandarasi wanafuata ratiba na miradi inakamilika kwa wakati uliopangwa
Hatua hiyo inalenga kuboresha miundombinu ya michezo nchini, huku maeneo mbalimbali yakiendelea na ujenzi, ukarabati na uboreshaji wa viwanja na vituo vya michezo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































