#Local News

MSAKO DHIDI YA BIASHARA HARAMU YA SUKARI UNAENDELEA KITALE

Mamlaka zimeimarisha msako dhidi ya biashara haramu ya sukari mjini Kitale, Kaunti ya Trans Nzoia, katika juhudi za kukabiliana na uuzaji wa bidhaa zinazokiuka sheria.

Operesheni hiyo inalenga kuwabaini wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara haramu ya sukari na kuhakikisha bidhaa zinazouzwa sokoni zinakidhi viwango na mahitaji yaliyowekwa na mamlaka husika.

Mamlaka zimewataka wafanyabiashara kuzingatia sheria na kanuni za biashara, huku hatua za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa dhidi ya watakaopatikana wakijihusisha na biashara hiyo haramu.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *