WATU 7 WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA AJALI YA NDEGE SAMBURU
Ndege aina ya Helikopta imeanguka katika eneo la Mlima Ololokwe, Kaunti ya Samburu, na kusababisha vifo vya watu wote saba waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini KCAA imethibitisha ajali hiyo, ikisema ilihusisha helikopta yenye nambari ya usajili 5Y-GYM.
Kwa mujibu wa KCAA, helikopta hiyo ilikuwa ikitoka Loisaba kuelekea Ewaso Nyiro ilipoanguka mapema leo huku uchunguzi ukitarajiwa kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































