KAMISHNA WA IEBC ANN NDERITU AONYA KUWA KAMPENI ZITAANZA MWEZI MEI MWAKA UJAO NA WALA SII SASA
Nchi imeingia katika kipindi cha kuongezeka kwa shughuli za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, ikisema ina vikwazo katika kushughulikia shughuli za kutafuta kura ambazo tayari zimeenea nchini.
Kamishna wa IEBC Ann Nderitu amesema kuchapishwa kwa ratiba ya uchaguzi katika Gazeti la Serikali Agosti 19 kuliashiria kuanza kwa mwaka wa uchaguzi, lakini hakumaanishi kuwa kipindi rasmi cha kampeni kimeanza.
Akizungumza katika kwenye mahojiano na runinga moja humu nchini Nderitu amesema kipindi rasmi cha kampeni kitaanza Mei 29, 2027, takriban miezi miwili kabla ya siku ya uchaguzi.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































