#Local News

MUTUSE ASIFIA MIRADI YA RAIS RUTO HUKO KIBWEZI

Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse amepongeza Rais William Ruto kwa hatua ya kupunguza bei ya mbolea, akisema hatua hiyo itawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa chakula.

Mutuse amesema kupunguzwa kwa gharama ya mbolea kutapunguza mzigo wa gharama za uzalishaji kwa wakulima, hasa wale wadogo, na kuwapa nafasi ya kuongeza uzalishaji wa mazao.

Amesema hatua hiyo pia inaweza kuchangia kuimarisha usalama wa chakula nchini na kuongeza kipato cha wakulima.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *