SIMAMA NA FAMILIA YA REX MASAI
Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amewataka Wakenya kusimama na familia ya Rex Kanyike Maasai, ambaye inasemekana aliuawa wakati wa maandamano ya jana Alham jioni.
Inasemekana kwamba Rex alipigwa risasi na kuuawa mwendo wa saa saba mchana katika barabara ya Moi avenue jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.
Akizungumza alipoungana na familia ya Rex katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City kabla ya upasuaji wa maiti, babu amesema amehuzunika kuona wazazi wakiwa katika majonzi kufuatia mkasa huo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































