THOMAS MULLER ANASTAAFU
Mshambulizi wa Ujerumani Thomas Muller alisema kuwa anastaafu kucheza soka la kimataifa baada ya michuano ya Euro 2024 ambayo timu mwenyeji ilitolewa katika robo fainali.
Muller, ambaye anatimiza umri wa miaka 35 mwezi Septemba, alikuwa kiungo muhimu wa timu ya Ujerumani iliyoshinda Kombe la Dunia la 2014.
MULLER mwenye mvuto pia alifunga bao la kwanza katika ushindi usiosahaulika wa Ujerumani wa mabao 7-1 dhidi ya wenyeji Brazil katika nusu fainali.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































