MACHAKOS: AFISA ALIANGUKA NA KUFARIKI AKIWA KATIKA NYUMBA YA KUPANGA
Afisa wa polisi katika Kituo cha Polisi cha Muungano amefariki baada ya kuanguka katika nyumba yake ya kukodi katika Kaunti ya Machakos.
Kulingana na ripoti ya polisi raia Evans Adango ameripoti kisa hicho baada ya mkewe, Polisi Konstebo Pauline Adenyoh kupata shambulio la kifafa.
Maafisa wa kituo cha Muungano wameelekwa eneo la tukio na kumkimbizwa Hospitalini kwa matibabu lakini alikuwa tayari ameaga dunia.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifathi maiti ukisubiri uchunguzi
Imetayarishwa na Janice Marete.
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































