POLISI UINGEREZA WACHUNGUZA MAUAJI YA MWANAMKE MKENYA ALIYEPATIKANA AMEUAWA LONDON
Polisi nchini Uingereza wanachunguza tukio la mwanamke mwenye asili ya Kenya aliyepatikana amepigwa hadi kufa katika nyumba yake eneo la Woolwich, Kusini Mashariki mwa London.
Taarifa ya Polisi wa Mijini imesema mwili wa Marianne Kilonzi, mwenye umri wa miaka 43, umepatikana katika nyumba yake baada ya wasiwasi kuhusu usalama wake kuripotiwa.
Kulingana na wasifu wake wa LinkedIn, Kilonzi, ambaye alikuwa mhitimu wa Sayansi ya Kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta, alihudumu kama makamu wa rais wa mauzo ya biashara na mtaji wa kazi katika benki kubwa ya kifedha, Citibank, kwa zaidi ya miaka 18.
Awali, alihudumu kama makamu wa rais wa hazina na suluhisho za kibiashara katika Citibank, Kenya, kwa karibu miaka miwili baada ya kuhudumu kama naibu makamu wa rais kwa takriban miaka 16.
Wapelelezi wamesema sababu ya kifo chake ni majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na kipigo kikali. Wanaamini kuwa Kilonzi alimfahamu mshambuliaji wake na wanamtafuta mshukiwa wa mauaji hayo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































