MUTUSE ASIFIA MIRADI YA RAIS RUTO HUKO KIBWEZI

Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse amepongeza Rais William Ruto kwa hatua ya kupunguza bei ya mbolea, akisema hatua hiyo itawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa chakula. Mutuse amesema kupunguzwa kwa gharama ya mbolea kutapunguza mzigo wa gharama za uzalishaji kwa wakulima, hasa wale wadogo, na kuwapa nafasi ya kuongeza uzalishaji wa mazao. Amesema hatua hiyo […]

KAMISHNA WA IEBC ANN NDERITU AONYA KUWA KAMPENI ZITAANZA MWEZI MEI MWAKA UJAO NA WALA SII SASA

Nchi imeingia katika kipindi cha kuongezeka kwa shughuli za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, huku Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, ikisema ina vikwazo katika kushughulikia shughuli za kutafuta kura ambazo tayari zimeenea nchini. Kamishna wa IEBC Ann Nderitu amesema kuchapishwa kwa ratiba ya uchaguzi katika Gazeti la Serikali Agosti 19 kuliashiria kuanza […]

MBUNGE WA MUKURWE-INI AFIKA MBELE YA NCIC

Mbunge wa Mukurwe-ini John Kaguchia amefika mbele ya Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano, NCIC, kujibu tuhuma za kutoa matamshi ya uchochezi. Mawakili wa Kaguchia wameiambia tume hiyo kuwa matamshi ya mteja wao yalinukuliwa nje ya muktadha aliokusudia, wakisisitiza kuwa hakuwa na nia ya kueneza chuki au kuchochea mgawanyiko miongoni mwa Wakenya. Kaguchia ameendelea […]

MGAO WA FEDHA ZA KAUNTI HATIMAYE UMEWASILI

Baraza la bajeti na uchumi baina ya serikali kuu na serikali za kaunti IBEC limepongeza wizara ya fedha kutoa kwa wakati fedha za kaunti za July na Agosti Akizungumza baada ya kikao cha 30 cha IBEC jijini Nairobi Naibu wa Rais profesa Kithure kindiki amesema amerithishwa na kupitishwa kwa sheria za mgao wa mapato kwa […]

BEI YA MBEGU ZA MAHINDI KUSHUKA KWA ASILIMIA 50 MWEZI UJAO.

Rais William Ruto ametangaza kuwa serikali itapunguza bei ya mbegu za mahindi kwa asilimia 50 kuanzia mwezi Septemba mwaka huu. Ruto amesema hatua hiyo itapunguza bei ya gunia la mbegu za mahindi kutoka bei  ya sasa sokoni ya Shilingi 300 hadi Shilingi 150. Akizungumza katika hafla ya ibaada, Kaunti ya Taita Taveta, Kiongozi wa Nchi pia amesema serikali […]

MAN CITY YAANZA ENZI MPYA KWA USHINDI WA KUSISIMUA

Manchester City imeanza maisha bila Pep Guardiola kwa ushindi wa dakika za mwisho, ikiilaza Bournemouth 2-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu chini ya kocha mpya Enzo Maresca. Bournemouth ilionekana kuelekea kuvuruga sherehe za City baada ya Marcus Tavernier kuifungia bao la kuongoza kipindi cha kwanza katika uwanja wa Etihad, lakini wenyeji wakaanza kurejea […]

FKF SUPER CUP: TUSKER YAANZA MSIMU KWA KUINYAMAZISHA GOR MAHIA

Tusker FC imeanza msimu wa 2026/27 kwa kishindo baada ya kuilaza Gor Mahia 3-1 na kutwaa taji la FKF Super Cup katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi. Francis Oduor, Engine Ikutwa na Ian Simiyu ndio walioipa Tusker mabao yake huku Ikutwa pia akiifungia Gor Mahia bao la kufutia machozi dakika ya 38, matokeo yaliyoipa Tusker […]

KABRAS YATWAA TAJI LA DRIFTWOOD 7S

Kabras Sugar imefanya mabadiliko ya kuvutia na kutwaa taji la Driftwood 7s baada ya kuwashinda mabingwa watetezi KCB kwa alama 15-5 katika fainali kali iliyochezwa Mombasa Sports Club\. KCB ilionekana kuelekea kutetea ubingwa baada ya Festus Shiasi kufunga jaribio dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza na kuwapa mabingwa hao uongozi wa 5-0 kabla ya […]

NDINDI NYORO AMTAKA MURKOMEN KUJIUZULU

Kiongozi wa chama cha PPK, Ndindi Nyoro, amemtaka Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, kujiuzulu akisema serikali imeshindwa kudhibiti kuongezeka kwa vurugu katika mikutano ya kisiasa nchini Akizungumza katika kaunti ya Murang’a Nyoro amesema licha ya serikali kuahidi kuwachukulia hatua wahusika na wafadhili wa ghasia hizo, hakuna aliyekamatwa hadi sasa Amesisitiza kuwa upinzani utaendelea kuwa na umoja kwa lengo la […]

UHURU: SITAKI KUITWA “SPONSOR”

Aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta amewataka wanasiasa kuacha kutumia nguvu kuzuia mikutano ya wapinzani kuelekea uchaguzi wa 2027, akisema badala yake wajielekeze kuuza sera na ilani zao kwa Wakenya Akizungumza katika Kaunti ya Trans Nzoia Uhuru amesema wananchi wanapaswa kupewa uhuru wa kuamua viongozi wanaowataka, bila wanasiasa kuwazuia wapinzani wao kufanya mikutano Uhuru pia amekanusha madai kuwa kurejea […]