NDINDI NYORO: SERIKALI IMEITELEKEZA ELIMU
Kiongozi wa chama cha PPK na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, ameisuta serikali kwa kuipuuza sekta ya elimu kwa kuchelewesha fedha za ufadhili wa shule, akisema hali hiyo inatishia maandalizi ya shule kwa muhula mpya
Akizungumza alipokutana na wajumbe katika makao makuu ya chama, Nyoro ameitaka serikali kutoa fedha za ufadhili wa shule kwa wakati ili kuhakikisha taasisi za elimu zinafunguliwa na kuendelea na shughuli bila vikwazo vya kifedha
Nyoro pia amezua hofu kuhusu usalama nchini, akisema kuenea kwa utamaduni wa kutumia wahuni katika siasa kunalipeleka taifa kwenye hali ya machafuko taratibu, na hivyo akataka hatua za haraka zichukuliwe kukomesha hali hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































