MALALAH ATAKA VIONGOZI WA UPINZANI WAAPE KUTOKUSALITI UMOJA
Naibu Kiongozi wa DCP Cleophas Malalah amewataka viongozi wote wanaolenga kuunda muungano wa upinzani kuweka ahadi ya wazi kwamba watabaki pamoja hadi mwisho wa safari.
Malalah amesema kila kiongozi anapaswa kutia saini ahadi binafsi ya kuendeleza umoja huo, hata iwapo hatateuliwa kuwa mgombea wa urais wa muungano, akisema hatua hiyo itajenga uaminifu miongoni mwa washirika.
Amesisitiza kuwa lengo kuu linapaswa kuwa ushindi wa upinzani katika uchaguzi wa 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































