UASU YAKATAA UAMUZI WA MOI UNIVERSITY KUWAPUNGUZA WAFANYAKAZI
Muungano wa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu UASU umeingia kupinga uamuzi wa uongozi wa chuo kikuu cha Moi wa kutangaza nafasi za kazi za wahadhiri 75 kuwa za ziada, hatua ambayo huenda ikawaacha wafanyakazi hao bila ajira.
UASU inashutumu chuo hicho kwa kile inachodai ni mpango wa kuwaondoa wahadhiri walioajiriwa kwa masharti ya kudumu na nafasi zao kuchukuliwa na wahadhiri wa muda.
Muungano huo umesema hatua hiyo ni kinyume cha sheria, isiyo ya kibinadamu na inageuza ajira za kitaaluma kuwa za muda, huku ukitaka uamuzi huo upitiwe na haki za wahadhiri zilindwe.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































