#Football #Sports

MANCHESTER CITY YAFIKIA MAKUBALIANO YA KUMSAJILI ALLAN

Manchester City imefikia makubaliano na Palmeiras kumnunua winga Allan, huku hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho huo zikiendelea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, City italipa euro milioni 40 kama ada ya msingi, pamoja na nyongeza zitakazotegemea masharti ya mkataba, huku nyaraka zikibadilishana kati ya vilabu hivyo.

Allan anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Enzo Maresca, huku uhamisho huo ukikaribia kukamilika baada ya pande hizo kufikia mwafaka kuhusu masharti ya dili hilo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *