#Local News

TAHADHARI YA KIAFYA

Umeshauriwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya magonjwa mbali mbali msimu huu wa sherehe ikiwemo kudumisha usafi na kuepuka maeneo yenye watu wengi ili kuepuka kuambukizwa au kueneza maambukizi.

Kupitia taarifa, katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni amesema ni kawaida kwa magonjwa ya kuambukizana kuenezwa msimu huu kutokana na watu kusafiri kwa wingi, mengi ya magonjwa yakienezwa kutokana na utangamano katika maeneo yaliyo na watu wengi, hewa chafu na chakula kilicho na viini.

Aidha, wizara hiyo imeshauri wakenya kuepuka kuhudhuria mikusanyiko iwapo wanahisi matatizo ya kiafya.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

TAHADHARI YA KIAFYA

WATAHINIWA WA KJSEA KUREKEBISHA SHULE

TAHADHARI YA KIAFYA

ODM YATOA MASHARTI KWA KENYA KWANZA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *