TERRY ENGESHA ATABIRI MABAO ZAIDI KWA POLICE BULLETS
Baada ya kuanza kampeni ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake kwa ushindi, mshambuliaji wa Kenya Police Bullets Terry Engesha anaamini timu hiyo bado ina mabao mengi zaidi ya kutoa katika mechi zijazo
Engesha amesema ushindi wa 2-1 dhidi ya vigogo wa Tanzania Simba Queens katika Uwanja wa Kigali Pele umeipa timu hiyo motisha zaidi, huku Police Bullets ikipanda kileleni mwa Kundi C.
Timu hiyo ya Rama Vijago ilipata ushindi katika mchezo uliokuwa na maamuzi kadhaa yenye utata kutoka kwa mwamuzi, lakini Engesha anaamini kadri mashindano yanavyoendelea, Police Bullets itaongeza makali mbele ya lango na kufunga mabao mengi zaidi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































