AFC LEOPARDS YAJIPANGA UPYA KWA MASHAMBULIZI YA UBINGWA
AFC Leopards imeonyesha azma mpya ya kuvamia taji la Ligi Kuu msimu wa 2026/27 baada ya kuwatambulisha zaidi ya wachezaji saba wapya pamoja na benchi jipya la kiufundi, wiki moja kabla ya msimu kuanza.
Miongoni mwa waliowasilishwa kwa mashabiki katika hafla ya utambulisho Jumamosi ni Kevin Luke Otiala na Sebastianos Wekesa, waliowasili kutoka Kariobangi Sharks, huku klabu ikilenga kuimarisha kikosi baada ya kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita.
Ingwe pia imepata huduma za Taddeo Lwanga kutoka Vipers ya Uganda na Adama Kanteh, huku Lwanga akitarajiwa kuleta uzoefu na nguvu zaidi katikati ya uwanja katika kampeni ya AFC Leopards ya kutafuta taji la ligi msimu huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































