WAKENYA WASHINIKIZA MSHIKAMANO, UMOJA
Wakenya kutoka matabaka mbali mbali wanaendelea kushinikiza mshikamano miongoni mwa viongozi ili kutuliza joto la kisiasa, ambalo wanahofia huenda likalemaza utendakazi wa serikali.
Akizungumza kwenye kaunti ya Nyandarua, Waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki amewahimiza viongozi kushirikiana kwa lengo la kuboresha Maisha ya wakenya.
Wakati uo huo, wananchi wa kawaida wamesikitishwa na mirengo ambayo imeibuka katika chama cha UDA, wakihofia kwamba huenda migawanyiko hiyo ikalemaza maendeleo na kuzua chuki.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































