#Local News

WAFANYAKAZI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU WAGOMA HUKO NANDI

Wafanyakazi wa mradi wa nyumba za bei nafuu katika eneo la Chesumei, Kaunti ya Nandi, wamegoma wakilalamikia kucheleweshwa kwa malipo yao kwa muda mrefu.

Wafanyakazi hao wamesema wameendelea kufanya kazi licha ya kutolipwa kwa wakati, hali ambayo wameeleza imewaweka katika changamoto za kifedha na kuathiri maisha yao.

Wameitaka kampuni inayohusika na mradi huo kushughulikia suala la malipo yao na kuhakikisha wanapokea mishahara na stahiki zao kwa wakati.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *