OKWARO ALENGA KUNG’AA AFCON NA KUINGIA KIKOSI CHA CHAN
Beki wa timu ya taifa ya Kenya chini ya miaka 20, Manzur Okwaro, analenga kung’aa kwenye mashindano ya AFCON kwa vijana na kupata nafasi katika kikosi cha CHAN.
Okwaro mwenye umri wa miaka 19, alicheza mechi yake ya kwanza kwa timu ya wakubwa dhidi ya Gabon baada ya kumvutia kocha Benni McCarthy.
Mchezaji huyo wa KCB anasema imani ya kocha McCarthy imempa motisha zaidi kuendeleza kipaji chake.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































