MURKOMEN: SERIKALI KUDHIBITI WIZI WA MIFUGO MARSABIT NA ISIOLO
Baadhi ya maafisa waandamizi wa usalama wakiongozwa na Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen wanatarajiwa kufanya mikutano hii leo katika kaunti za Marsabit na Isiolo ili kuweka mikakati ya kudhibiti hali ya usalama kufuatia ongezeko la visa vya wizi wa mifugo.
Waziri Murkomen amesema serikali imedhamiria kukabiliana vilivyo na wahalifu na kuhakikisha amani inarejea katika maeneo hayo yanayoathirika mara kwa mara na machafuko.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































