JORGE FRUTOS KUJAZA PENGO LA YAMAL “LA ROJA”
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uhispania maarufu kama La Roja Luis de la Fuente, amemteua wing’a wa Rayo Vallecano Jorge de Frutos kujaza pengo la Lamine Yamal kutokana na jeraha katika maandalizi ya kusaka tiketi ya kuelekea Marekani mwaka ujao kwa mashindano ya kombe la dunia.
Kumekuwa na vuta nikuvute baina ya timu hiyo na klabu ya Barcelona yake Yamal kuhusiana na jinsi klabu hiyo imeshughulikia jeraha la kinda huyo.
Uhispania inajiandaa kwa mechi za mwisho dhidi ya Georgia na Uturuki, ambako inasaka tiketi ya kusakata dimba la dunia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































