#uncategorized

GOR WAONYESHA UBABE KASARANI

Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya soka KPL Gor Mahia walitoka chini na kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Murang’a SEAL ugani Kasarani kwenye mechi ya ligi kuu hapo jana, na kupanda kileleni kwa jedwali kwa pointi 30 sawa na AFC Leopards.

Gor waliporomoka ndani ya dakika 18 za mwanzo za mchezo na kuruhusu mabao ya haraka, Murang’a SEAL wakitishia kuendeleza rekodi rekodi yao ya mechi 11 bila kupoteza.

Mabao ya Joe Waithira na Francis Memusi yaliwatia baridi mashabiki wa Gor, ila vijana mabingwa hao walikataa kuachia na kurejea kwa kishindo katika kipindi cha 2.

Felix Oluoch alitumia nafasi ya makosa wa kipa wa SEAL Mustapha Oluoch aliyetema mpira na kuwarejesha K’Ogalo mchezoni kabla ya Paul Ochuonga kusawazisha.

Kocha mkuu Charles Akonnor alifanya mabadiliko kadhaa ya kimfumo na kuwaleta mchezoni wachezaji kadhaa akiwemo Ebenezer Assifuah aliyefunga bao la ushindi.

Katika matokeo mengine, rekodi ya kutoshinda kwa Police FC iliingia mechi ya 5 kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Mara Sugar, ambao pia sasa wamecheza mechi 4 bila ushindi.

KCB FC watamenyana na Nairobi United hii leo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

GOR WAONYESHA UBABE KASARANI

SIKU KUBWA UGANDA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *