#Football #Sports

HARAMBEE STARS KUCHEZA FIFA SERIES RWANDA

Harambee Stars watasafiri kwenda Rwanda kushiriki mashindano ya kwanza ya FIFA Series katika dirisha lijalo la kimataifa linaloanza Jumatatu, Machi 23, kwa mujibu wa uthibitisho wa FIFA.

Shirikisho la Soka Kenya (FKF) limethibitisha kuwa Kenya imepangwa Kundi A pamoja na Estonia, Grenada na wenyeji Rwanda.

FIFA Series ni mpango wa kimataifa unaolenga kuongeza ushindani na kuwapa timu za taifa nafasi ya kucheza dhidi ya wapinzani kutoka mashirikisho tofauti ya soka duniani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *