#Local News

NATEMBEYA AITAKA SERIKALI KUSAIDIA WAKULIMA

Gavana wa kaunti ya Trans Nzoia, George Natembeya, ameitaka serikali ya kitaifa kushirikiana na kaunti kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa bei nafuu ili kuimarisha sekta ya kilimo.

Akizungumza katika wadi ya Hospital wakati wa hafla ya kugawa mbegu kwa zaidi ya wakulima elfu kumi, Natembeya amesema serikali yake imefanikiwa kuwafikia zaidi ya wakazi laki tatu kwa mbegu bila malipo licha ya changamoto za kiuchumi, hususan upatikanaji wa mbolea.

Viongozi wa eneo hilo pia wamewahimiza wanasiasa kuzingatia masuala muhimu yanayowakabili wananchi kama hali ngumu ya maisha ili kusaidia kupunguza mzigo kwa Wakenya wa kawaida.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

NATEMBEYA AITAKA SERIKALI KUSAIDIA WAKULIMA

VIFO VYA MAFURIKO VYAFIKIA 88

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *