#Local News

WAUGUZI  WAENDELEA NA MGOMO NAIROBI

Wauguzi kupitia muungano wao wameendeleza mgomo katikati mwa jiji la Nairobi kushinikiza kutekelezwa kwa mkataba wa makubaliano CBA wakisisitiza kwamba hawatarejea kazini hadi pale malalamiko yao yatakaposhughulikiwa kikamilifu

Mgomo huo umedumu kwa siku 29 sasa kote nchini huku wauguzi wakishinikiza utekelezaji wa CBA, kulipwa kwa malimbikizi ya madeni, muongozo bora wa kuhudumu,pamoja na kurekebishwa kwa mfumo wa malipo kwa wahudumu wa afya ya umma UHC miongoni mwa maswala mengine.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *