#Local News

WAKAAZI BUSIA WARAIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA UMEME

Wakazi wa vijiji mbalimbali katika Kaunti ya Busia wamehimizwa kulinda na kutunza miundombinu ya umeme inayojengwa katika maeneo yao na taasisi za umma, zikiwemo shule, vituo vya afya na masoko.

Wito huo umetolewa huku visa vya wizi wa nyaya na vifaa vya umeme vikiongezeka katika Kaunti ya Busia, hali inayoweza kuchelewesha au kuhujumu juhudi za kusambaza umeme kwa wananchi.

Wakazi wameombwa kushirikiana na mamlaka husika na kuripoti mara moja visa vya wizi au uharibifu wa miundombinu ya umeme ili kuhakikisha miradi hiyo inalindwa na wananchi wanaendelea kunufaika na huduma ya umeme.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *