POLISI KAKAMEGA WAKABILIANA NA KUNDI LA WATU WENYE NJAA YA MAFUTA
Polisi wamekabiliana na kundi la watu katika mapigano huku wakichota mafuta kutoka kwa lori lililopinduka katika barabara ya Eldoret-Webuye kaunti ya Kakamega.
Kwa mujibu wa polisi, umati huo ulikuwa umefika eneo la tukio wakiwa wamejipanga kwa vifaa vya kubebea mafuta bila kujali usalama wao.
Lori hiyo iliyokuwa imebeba takribali lita elfu 39,000 za mafuta ya petroli ilipinduka katika eneo la Mukhonje baada ya dereva kupoteza udhibiti wake usiku wa kuamkia leo ilipokuwa ikisafirisha bidhaa hiyo kutoka Eldoret hadi Malaba.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































