#Local News

TUTAWATIBU MKIUMIA KATIKA MAANDAMANO; USHIRIKA WA MATIBABU 

Huku maandamano ya Occupy Bunge yakiingia siku ya pili, Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya (KMPDU)  umetangaza kushiriki kwa wanachama wake, kwa mpango wa kutoa huduma za matibabu kwa waandamanaji.

Katibu Mkuu wa KMPDU Davji Atellah amesema madaktari watashughulikia watakaopata majeraha kwa dharura ambazo zinaweza kutokea kutokana na maandamano yaliyopangwa katika miji yote ya Kenya.

Madaktari hao wananuia kukusanyika Nairobi na miji mingine mchana kuungana na waandamanaji wengine.

Imetayarishwa na Janice Marete

TUTAWATIBU MKIUMIA KATIKA MAANDAMANO; USHIRIKA WA MATIBABU 

USHURU KWA SODO? JAMANI!!!!

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *