RUTO AMHAKIKISHIA JUMWA WADHIFA SERIKALINI
Rais william Ruto amemhakikishia aliyekuwa Waziri wa jinsia Aisha Jumwa kwamba hatamuacha nje ya serikali yake licha ya kumtimua kutoka baraza la mawaziri.
Rais ametoa hakikisho hilo akiwa kwenye ziara ya maendeleo katika kaunti ya Kilifi, ambako Jumwa amempongeza rais kwa kuwatetua mawaziri wawili kutoka mwambao wa pwani.
Aidha, Jumwa ameahidi kushirikiana na mawaziri hao kuhakikisha maslahi ya wakazi yanaangaziwa.
Naye rais Ruto amesema ana matumaini katika mawaziri aliowateua kutoka eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































