GACHAGUA AKATAA KUGAWA NGOME ZA KISIASA ZA UPINZANI
Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua amepinga wito wa kugawana maeneo yenye ushawishi wa kisiasa miongoni mwa vyama vya United Opposition, akisema ushindani wa ndani ya upinzani unaweza kuleta mwamko mkubwa zaidi wa wapiga kura kuelekea uchaguzi wa 2027.
Gachagua amesema kila chama kinapaswa kuwa na nafasi ya kutafuta uungwaji mkono katika maeneo mbalimbali bila kuweka mipaka ya kisiasa, akidai ushindani huo unaweza kuongeza hamasa na hatimaye kuinua idadi ya Wakenya watakaoshiriki uchaguzi wa urais.
Gachagua amesisitiza kuwa licha ya ushindani wa ndani, Muungano wa Upinzani bado utaungana nyuma ya mgombea mmoja wa urais dhidi ya Rais William Ruto mwaka 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































