ATWOLI AMSUTA UHURU KWA KUJARIBU KUGAWANYA MAGHARIBI
Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli ametoa madai mazito ya kisiasa, akimtuhumu aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta kwa kumfadhili Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna katika kile anachodai ni juhudi za kugawanya kura za eneo la Magharibi kuelekea uchaguzi wa 2027.
Akizungumza Kakamega, Atwoli amedai kuwa Uhuru anafadhili shughuli za Sifuna pamoja na vuguvugu la Linda Mwananchi, akishirikisha pia Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, kwa lengo la kudhoofisha mshikamano wa kisiasa wa eneo hilo.
Atwoli amesema hatua hiyo inaweza kuvuruga umoja wa kisiasa wa Magharibi mwa Kenya, huku akiwataka viongozi na wananchi wa eneo hilo kuwa macho dhidi ya mipango anayodai inalenga kuwagawa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































